UWEKAJI VIGINGI PORI LA LOLIONDO HAUTOATHIRI MAENDELEO YA WANANCHI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la uwekaji wa vigingi katika eneo la kilometa za mraba 1,500 la Pori Tengefu la Poloreti-Loliondo ambalo limekamilika kwa asilimia 100 halitoathiri maendeleo ya wakazi waishio kwenye eneo la vijiji 14 vinavyopakana na eneo hilo. Hata hivyo, Mheshimiwa Majaliwa amesisitiza kwamba hakutakuwepo na kijiji chochote kitakachofutwa na hakuna miundombinu itakayoondolewa kwa kuwa ndani ya eneo la kilometa za mraba 1,500 hakuna miundombinu yoyote. Ameyasema hayo leo